Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

National Ranching Company Limited - NARCO

News

UZINDUZI WA VITENDEA KAZI VYA SHAMBA


Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kiasi cha shilingi bilioni 4.65 kwa ajili ya kununua vitendea kazi na ng'ombe wazazi ili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa kampuni hiyo.

Mhe.Ulega amesema lengo la Rais, Dkt. Samia ni kuiimarisha NARCO kwa kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili waweze kunenepesha ng'ombe, kuimarisha biashara ya nyama bora ya Kongwa Beef na kuzalisha malisho ya mifugo kwa wingi na kuyauza ndani na nje ya nchi.

"Hivi sasa tumeshafika katika kiwango cha kuuza nje ya nchi nyama tani elfu 12, na kuanzia mwaka ujao na kuendelea tutatoka kwenye tani elfu 12 na kutafuta tani elfu 50 na ikiwezekana mpaka tani laki moja"-Mhe.Ulega

Aidha, amesema serikali ina mipango ya kuanzisha skimu za umwagiliaji wa malisho, ili yaweze kuzalisha kwa wingi kwa ajili ya kuyauza ndani na nje ya nchi.

"Kama ambavyo huwa tunasafirisha mahindi kutoka maeneo mbalimbali na kuwapelekea wahitaji tunataka pia tuzalishe malisho kwa wingi na kuyasafirisha kuyapeleka kwa wahitaji waliopo ndani na nje ya nchi"Ulega amefafanua

Hayo yamefahamika wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega aliyoifanya katika Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilayani Kongwa, Jijini Dodoma.

Waziri Uleha amezindua Matreka mapya matano (5) na kupokea ngo'mbe elfu moja (1000) kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa kampuni ya NARCO, Mhe. Ulega alimshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha kampuni hiyo ili iweze kujiendesha kibiashara.